Misri imetumia Helicopter kufanya
mashambulizi ya mizinga dhidi ya wakereketwa wenye imani kali walio katika eneo
la Sinai tangu mwaka 1973 katika kile jeshi la Misri lililochotaja kama shambulio la kurejesha utulivu.
Matumizi ya anga ni ishara ya mabadiliko ya vita
vya Misri dhidi ya wakereketwa wa Kiislam ambao wamezidisha shughuli zao katika
eneo lenye milima na jangwa lenye mpaka na Israili na Gaza.
Mapema wiki hii wapiganaji wakereketwa
waliishangaza Misri kwa ujasiri wao kwa shambulizi ambamo askari 16 waliuawa,
magari ya jeshi yakaibwa na kuelekea Israel kwa lengo la kujaribu
kufanya shambulio jingine.
Katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya
taifa jeshi limesema kua limeanzisha operesheni ya mchanganyiko wa vikosi kwa
kutaka kurejesha utulivu huko Sinai, majeshi yakiungwa mkono na Jeshi la anga.
Shambulio la siku ya jumapili ndio baya kuwahi
kufanywa huko Sinai kwa miaka mingi na hatari kuliko yote dhidi ya vikosi vya
Misri ikiashiria ongezeko la vitendo vinavyokiukaq sheria katika eneo hilo.
Katika tukio la hivi karibuni, watu wenye silaha
waliwafyatulia risasi walinzi kwenye vizuizi huko El -arish, mji mkuu wa Wilaya
ya Sinai, mji ulio umballi wa kilomota 50 kutoka mpaka wa Gaza na Israili.
Ghasia kwenye mpaka wa Israel na Misri inaweza kutishia
mkataba wa amani baina ya nchi hizi mbili.
Hio ndio sababu Israel imeiambia Misri ichukue
hatua za kusuluhisha vurugu badala yake kupeleka vikosi vyake. Israel
imekubali kuondoa baadhi ya masharti yanayozuwia shughuli za kijeshi katika
Sinai ili Wa Misri waweze kuingiza vikosi zaidi.
Lakini uvamizi wa Misri dhidi ya kile walichokiita
magaidi hautobadili lolote katika sehemu ya Sinai inayokaliwa na makabilia ya
Wa Bedwini wenye fikra huria.
Ni eneo linalovutia kwa makundi ambayo yangependa
kutumia sehemu isiyokua na utaratibu wowote wa uongozi kwa aijili ya kuifika
Israili.
Rais wa Misri Mohammad Mursi aliahidi kwamba atadhibiti eneo la Sinai kwa ukamilifu.
chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment