1107.7 UPENDO FM RADIO LIVE

UPENDO FM LIVE

Saturday, September 8, 2012

MADHIMISHO YA MIAKA 125 YA INJILI-KILELE KISARAWE

 Wageni mbalimbali wakifuatilia ibada ya Kilele cha Jubilei ya miaka 125 ya injili katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Ibada ya Kilele ilifanyika Kisarawe, sehemu ambayo Mmisionari wa kwanza Mch. Johan Jacob Greiner aliweka makazi yake na kujenga kanisa la kwanza la kiinjili.
 Katika ibada hiyo kulikuwa na matendo mbalimbali, ikiwemo Ibada ya kuwabariki watheolojia kuwa wachungaji, iliyofanywa na Mkuu wa KKKT Askofu Dakta A.G.Malasusa
 Wachungaji wapya wakibarikiwa
Mchungaji mpya akivishwa Stola,,kama alama ya kuruhusiwa kufanya kazi za kichungaji, aliyeshika kipaza sauti ni Msaidizi wa askofu Dean G.P.Fupe.,,picha zipo nyingi, tutaendea kuwaletea picha za tukio hili la aina yake, ambalo lilivutia wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi, (Picha zote na Isaac Kikula wa Upendo Fm Radio?