Kisarawe- Mji wa Kisarawe una changamoto nyingi, lakini changamoto kubwa ya kisarawe ni ukosefu wa maji. serikali inatakiwa kuangalia namna ya kutatua tatizo hili ambalo linawatesa wananchi wa Kisarawe kwa miaka nenda rudi.
Huyu ni mmoja wa wakazi wa Kisarawe, hapa akifurahia baada ya timu ya Upendo Fm radio kumpa fedha kwa ajili ya kununulia mafuta ya taa. Kwa nyuma ni KKKT Usharika wa Kisarawe Mjini.
Mkuu wa Jimbo la Kusini Magharibi Mch Mika Kitale akihojiwa na Isaac Kikula wa Upendo Fm kuhusu masuala mbalimbali ya Kisarawe na Jimbo lake.
Mzee Samwel ambaye Upendo Fm ilifika nyumbani kwake kwa ajili ya kupata mawili matatu kutoka kwa mkongwe huyo wa mji wa Kisarawe. Mzee Samwel bado ana nguvu ya kuendesha baiskeli kutoka Kisarawe hadi Dar es Salaam, na tena baiskeli yake haina hata break, ni mzee mkweli na mcheshi pia.
Jopo zima la Upendo Fm Radio likiwa nyumbani kwa mzee Samwel, Kisarawe kwa ajili ya kupata habari mbalimbali za kihistoria.
Hapa ni Meneja wa Upendo Fm Radio Bi Agatha Lema (katikati) akiwa kwenye ziara ya kutembelea wasikilizaji wa vijijini, hapa yuko Kisarawe nyumbani kwa mzee Samwel.