Baaadhi ya watoto wa wachungaji wa KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani wakiwa kwenye hafla yao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Azania Front jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Na Isaac Sifa Kikula,
Dar es Salaam.
Watoto wa wachungaji wametakiwa
kuwa mfano wa kuigwa kwa kuishi maisha ya heshima, adabu, busara na utii na
kujifunza kwa maisha ya Yesu Kristo ili waweze kufanyika Baraka katika jamii.
Akifungua hafla ya watoto wa
wachungaji ambayo imefanyika kwenye ukumbi wa Azania Front jijini Dar es Salaam leo,
Mchungaji ASTON KIBONA amewasisitizia watoto hao kuwa tabia zao zinatakiwa
kutofautiana na tabia za watoto wengine wasio wakristo.
Watoto wa wachungaji wa KKKT-DMP katika hafla hiyo, aliyeshika kitambaa kati ni mtoto wa askofu Dr A. Malasusa.
Ian M. Lema, akiwasalimia wenzake kwenye hafla hiyo
Mke wa Askofu Malasusa, Bibi Erica Malasusa, akizungumza na watoto wa wachungaji wa kanisa hilo
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mke
wa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu Dakta ALEX MALASUSA,
Bibi ERICA MALASUSA amewaambia watoto hao kuwa licha ya changamoto za kukua kwa
teknolojia ikiwemo matumizi ya runinga, redio, magazeti na intaneti, watoto
wanatakiwa kumfanya Yesu Kristo kuwa ndiye mfano wao wa kuufuata.