Wakuu wa Sudan wanasema watu
kadha wamekufa kwenye shambulio lilofanywa na wapiganaji dhidi ya
wanajeshi wa serikali katika eneo la Darfur, magharibi mwa nchi.
Afisa mmoja wa serikali alisema wanamgambo
wanaounga mkono serikali wameuliwa katika shambulio hilo la ghafla,
karibu na al-Fasher, mji mkuu wa jimbo la North Darfur.
Umoja wa wapiganaji - Sudanese Revolutionary
Front - ulisema ulifanya shambulio hilo na kuuwa wanajeshi wa serikali
na kuteka magari ya jeshi na silaha.
Baadhi ya makundi ya wapiganaji ya Darfur mwaka
jana yalitia saini mkataba wa amani na serikali ya Sudan, lakini makundi
mengine yanaendelea kupigana.