Washarika mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Sadaka zinatolewa, sadaka ya mavuno hutolewa mara moja tu kwa mwaka.
Wengi hupenda kumtolea Mungu sehemu ya mali zao, kama mifugo, mazao, bidhaa za dukani n.k
Wakati wengine wakihamasishana kuharibu au kuchoma majengo ya kuabudia, sisi tunaendelea kuwahamasisha watoto wetu kujenga tabia ya utoaji.Watoto walikuwa sehemu ya watu waliotoa sadaka yao ya Mavuno
Radio Upendo ilirusha moja kwa moja Ibada hiyo, na hapo ni fundi mitambo Mkuu Fred Kissinda, Fundi msaidizi Eliapendavyo Estomih na mwenye tai nyekundu nyuma yao ni mtangazaji Isaac Kikula wa Upendo Fm Radio.
Kwaya ya Uinjilist Kijitonyama iliwasha moto katika Ibada hiyo iliyofanyika kwenye kiwanja kipya kinachotarajiwa kujengwa kanisa kubwa la KKKT Usharika wa King'ongo.
FFundi mitambo fred Kissinda akiwajibika
IIbada iliendeshwa na Msaidizi wa askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dean G.P. Fupe,,hapa akibadilisha sadaka za mavuno kuwa kwenye thamani ya fedha.
KKuku, bata, mbuzi na vinginevyo vilivyotolewa vilinadiwa na fedha kuwekwa kwenye mfuko wa kanisa. Picha zote na Isaac Kikula wa Upendo Fm Radio.