Kufuatia ajali ya meli iliyotokea kwenye bahari ya Hindi jana, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda ameahirisha kikao cha leo ili kuwapa wabunge fursa ya kushiriki mazishi na maombolezo. Baada ya wabunge kuingia ndani ya ukumbi, walipata fursa ya kusimama dakika moja, maalum kwa ajili ya kuwakumbuka waliokumbwa na maafa hayo.
Wednesday, July 18, 2012
UOKOAJI NA UOPOAJI
Waokoaji wakiendelea na jitihada za uokoaji kufuatia kuzama kwa meli katika bahari ya Hindi,,kwa mujibu wa taarifa rasmi, watu 25 wamefariki kwenye ajali hiyo.
Waokoaji wakiendelea kusaka majeruhi na miili ya waliofariki, inadaiwa kuwa jana hali ya hewa kwenye bahari ya Hindi haikuwa nzuri na ndio chanzo cha ajali hiyo.
Raia wa kigeni nao walikuwemo kwenye meli hiyo. Habari na Picha toka mitandao mbalimbali.
MELI ILIYOKUWA IKITOKEA DAR KWENDA ZANZIBAR YADAIWA KUZAMA
KUNA TAARIFA KWAMBA MELI MOJA ILIYOKUWA IKITOKEA DAR KWENDA ZANZIBAR IMEZAMA IKIWA NA ABIRIA 200 NDANI YAKE,,TUOMBE MUNGU KIKOSI CHA UOKOZI KIWAHI KUFIKA ENEO LA TUKIO
JK AMPOKEA RAIS WA LIBERIA
Ni yule mwanamama wa kwanza Afrika kuwa Rais,,yuko nchini kwa ziara rasmi na atafanyiwa dhifa ya kitaifa.
Subscribe to:
Posts (Atom)