Bofya link hii
http://www.elct.org/news/2012.06.003.html
Friday, July 13, 2012
WAKATI JK AKIHUDHURIA MKUTANO WA UZAZI
UELEWA mdogo wa
wananchi juu ya elimu ya uzazi wa mpango umebainishwa kuwa ni sababu ya ongezeko la vifo
vya akinamama vinavyotokana na uzazi.
MRATIBU wa uzazi
wa mpango kutoka Wizara ya Afya na ustawi wa jamii nchini Maurice Hiza amesema
hayo wakati akitoa mada katika kilele cha maadhimisho ya siku ya idadi ya
watu duniani iliyofanyika kitaifa Mkoani Morogoro iliyowahusisha watumishi mbalimbali
wa serikali, viongozi wa dini, wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari na
wanachuo kutoka vyuo vikuu.
Hiza alisema kuwa
uzazi unapopangiliwa vizuri hupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga.
Aidha Hiza
alisema kuwa kiwango cha utumiaji wa njia za uzazi wa mpango nchini bado upo
chini ambapo alisema kuwa asilimia 25 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa
ambao wangependa kupumzika au kupangilia lakini hawafuati njia yoyote ya uzazi
wa mpango na hivyo kujikuta wakiingia katika matatizo ya uzazi ikiwa ni pamoja
akupoteza maisha.
Hata hivyo
alisema kuwa nchi ikiwekeza kwenye uzazi wa mpango hupata faida kubwa
kiafya,kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla .
Subscribe to:
Posts (Atom)