Na Isaac Sifa Kikula,
Dar es Salaam.
Waziri Mkuu MIZENGO PINDA
amesema serikali haipangi vipaumbele vya maendeleo kwa kuzingatia vigezo vya
dini.
Amesema madhumuni ya
kufanya sensa ni kuiwezesha serikali kupanga vipaumbele vya maendeleo na kwamba
uwepo wa kipengele cha dini kwenye hojaji za sensa kungeleta hisia za kidini
kwenye upangaji wa vipaumbele vya maendeleo.
Waziri Mkuu PINDA amesema
hayo asubuhi hii wakati akijibu maswali ya papo kwa papo ya waheshimiwa wabunge
bungeni mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment