KAULI iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwamba hakuna ushahidi wa kuwashtaki watuhumiwa rushwa ya rada, inaonekana kumfunga mdomo Waziri wake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ambaye aliwahi kuahidi kwamba angewataja watuhumiwa hao.
Rais Kikwete alipokutana na wakuu wa vyombo vya habari wiki iliyopita, alisema Serikali inashindwa kuwashtaki waliotuhumiwa katika suala hilo kutokana ukweli kwamba hata Uingereza walikana Kampuni ya BAE Systems kutoa rushwa na badala yake wakasema ilikosea katika kuandika hesabu zake.
Wakati Rais Kikwete akisema hakuna ushahidi wa kuwashtaki watuhumiwa wa rushwa ya rada, tayari Membe alikuwa amesema watuhumiwa wapo, anawajua na aliahidi kwamba angewataja bungeni.
Hata hivyo, Membe aliyewasilisha Hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya wizara yake bungeni juzi, alishindwa kutekeleza ahadi yake licha ya kutakiwa kufanya hivyo na baadhi ya wabunge, wakiongozwa na Waziri Kivuli wa wizara hiyo, Ezekia Wenje ambaye pia ni Mbunge wa Nyamagana (Chadema).
Juzi, kabla Membe hajasoma hotuba yake, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alitoa taarifa rasmi ya Serikali bungeni kuhusu suala hilo na alisema kuwa, hakuna mtuhumiwa wa rada anayeweza kupelekwa mahakamani na kutamka kwamba mjadala kuhusu suala hilo umefungwa rasmi.
story nzima soma www.mwananchi.co.tz
Chanzo;mwananchi
Comments za wasomaji
Ushahidi unakosekanaje hata kabla ya uchunguzi kufanyika?
Kwa nini Kikwete ndiye wa kutoa uamuzi wakati mahakama ndio zinazosimamia
masuala ya sheria?
Kikwete na wenzake ndio wahusika wa rada, kwa nini anamzima
membe mdomo au ndio anataka kumfagilia Lowasa na Chenge kwenye uchaguzi mwaka
2015 wa Urais?
Mwandishi, kuna tofauti kati ya "ushahidi" wa
kimahakama na "ushahidi" wa kisiasa. Kamwe usichanganye sheria na
siasa!!
Katika hii nchi yetu, ni ukweli usiopingika huyu Raisi wetu
ndiye fisadi namba moja... maana kila kitu anajaribu kuuficha ukweli ...!!
JK anatakiwa aelewe kuwa watanzania anaowaongoza sio wale
walioongozwa na JK miaka ya sabini
Jifurahishe lakini naamini ipo siku maskini wakitanzania ataweza kunywa uji wenye sukari
Jifurahishe lakini naamini ipo siku maskini wakitanzania ataweza kunywa uji wenye sukari
Nafikili cha muhimu ni sisi wananchi kuamua kuwachagua
viongozi wazalendo na sio wapenda magendo.
Mbuzi wa bwana heri na shamba la bwana Heri hivyo si ajabu
Bwana Heri [NENO BAYA]liza mjadala huo.
No comments:
Post a Comment