Viongozi wa mataifa ya eneo la maziwa makuu walioko mjini Kampala kwa kikao cha
kutafuta suluhisho la mzozo wa kivita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo, wamekubaliana kuunda jeshi la pamoja kulinda usalama katika eneo la
mashariki mwa DRC.
kutoka kushoto; Rais Paul Kagame wa Rwanda, Jakaya Kikwete wa Tanzania, Yoweri Museveni wa Uganda na Joseph Kabila wa DRC kwenye kikao kilichofanya uamuzi huo, Kampala Uganda.
Baada ya kikao kilicho kufunguliwa jana na rais Yoweri
Museveni wa Uganda na kuhudhuriwa na marais watano kutoka mataifa ya eneo la
maziwa makuu ni moja ya mikakati ya kumaliza mzozo wa mashariki mwa Kongo.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Kampala, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa
Uganda Oriem Okelo, amesema mataifa wanachama yamekubaliana kubuni jeshi la
pamoja kulinda amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Lakini
amesema mawaziri wa ulinzi kutoka mataifa hayo watakutana kuchukuwa uamuzi wa
mwisho kuhusu kubuniwa kwa jeshi hilo.
Wahenga walisema vita haina macho. Vita vinavyoendelea Mashariki mwa DRC vimesababisha maelfu kukimbia makazi yao.
''kikosi
kitakachobuniwa kitakuwa kama kile cha Umoja wa Mataifa au Umoja wa Afrika na
ni sharti Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zikubaliane,'' amesema Bw.
Okelo.
Mkutano
huo wa mawaziri wa ulinzi utafanyika tarehe 15, mwezi huu wa Agosti.
Bwana
Okelo amesema marais wa Rwanda Paul Kagame na Joseph Kabila wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo wameafikia makubaliano na sasa ''wanazungumza kwa simu na
hawana matata.''
Mwenyekiti
wa kikao hicho cha viongozi wa eneo la maziwa makuu rais wa Uganda Yoweri
Museveni alifanya kikao cha faragha na Bw. Kagame anayeshutumiwa na baraza la
usalama la umoja wa mataifa kwa kutoa msaada kwa waasi wa M23 katika eneo la
mashariki mwa DRC.
Kiongozi wa kisiasa wa kundi la M23
Kadhalika
alifanya mashauri na Bw. Kabila.
Kabla
ya kikao hicho kinachokamilika leo hii kuanza, Bw. Museveni, baada ya ufunguzi
rasmi aliwaagiza waandishi wa habari kuondoka mara moja na pia kuliagiza
shirika la utangazaji nchini Uganda UBC kutopeperusha yale yaliyokuwa
yakijadiliwa katika mkutano huo moja kwa moja.
Mwandishi
wa BBC mjini Kampala anasema hiyo ni dalili kuwa huenda kulikuwa na ubishi
mkali katika mkutano hu
No comments:
Post a Comment