Kiongozi mpya wa kanisa katoliki duniani anasubiriwa na majukumu mazito
katika bara la Afrika licha ya waumini wa kanisa hilo kuongezeka kwa
kasi kubwa katika bara hilo.
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani papa Benedicto wa 16 anaondoka rasmi
madarakani leo (28 Februari), wakatoliki barani Afrika wanasubiri kwa
hamu kujua ni nani atakayerithi kiti hicho. Pamoja na kwamba kuna
waumini wengi wa kanisa hilo lakini pia changamoto ni nyingi
zinazomsubiri kiongozi mpya wa kanisa hilo.
Kushoto Papa Benedict wa 16 wakati akiwaaga makadinali. Baadhi ya makadinali wanaopewa nafasi ya kuchaguliwa kuwa Papa
Ikiwa takwimu zinabidi kuzingatiwa basi kanisa Katoliki halina cha
kuhofia barani Afrika, kwani katika mwaka 2011 idadi ya waumini wa
kanisa hilo kote barani humo ilionekana kuongezeka kwa zaidi ya milioni 6
na kufikia watu milioni 18. Warsha zinazotoa mafunzo ya upadre kwa
kizazi kipya zinaonekana kufurika bila kikomo wakati nchi zinazokabiliwa
na mizozo barani humo kama vile Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo au
Sudan Kusini mara nyingi mapdri wakikatoliki wanajikuta wakiwa na sauti
kuliko wajumbe wa serikali.
No comments:
Post a Comment