Kufuatia ajali ya meli iliyotokea kwenye bahari ya Hindi jana, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda ameahirisha kikao cha leo ili kuwapa wabunge fursa ya kushiriki mazishi na maombolezo. Baada ya wabunge kuingia ndani ya ukumbi, walipata fursa ya kusimama dakika moja, maalum kwa ajili ya kuwakumbuka waliokumbwa na maafa hayo.
No comments:
Post a Comment