1107.7 UPENDO FM RADIO LIVE

UPENDO FM LIVE

Monday, February 25, 2013

AJALI YA MWAKA 2013 IRINGA

Hii ilikuwa iringa hivi karibuni. ni kama moja lilibebwa likapandishwa kwenye gari lingine

Saturday, December 8, 2012

TASWIRA MBALIMBALI ZA MKUTANO MKUU WA KKKT-DMP ULIOMALIZIKA HIVI KARIBUNI


 Wajumbe wakuinga mkono moja ya hoja zilizojadiliwa
 Wachungaji Wanawake wa KKKT-DMP wakipata picha ya pamoja na Baba Askofu Malasusa na Askofu Mstaafu E. Sendoro

Meza Kuu ikipitia kabrasha kwa makini wakati Meneja wa Upendo Fm Radio Agatha Lema akiwasilisha taarifa ya kituo hicho kinachomilikiwa na KKKT-DMP
 Wa kwanza kushoto ni Bishop Malasusa katikati ni Katibu Mkuu wa DMP Balozi Richard Mariki na mwisho ni Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Marekani Bishop John Bradosky

 Tabasamu kutoka meza kuu
 Picha ya pamoja ya wajumbe mbalimbali

 Wajumbe wa mkutano wakimsifu Mungu kwa hisia
 Hapa Msaidizi wa Askofu wa DMP Mchungaji G.Fupe akitoa neno la shukrani baada ya kuteuliwa kwa mara nyingine kushika wadhifa huo na kuthibitishwa na mkutano mkuu
 Hapa akipongezwa na Baba Askofu Malasusa
 Hongera sana.
Katibu Mkuu, Askofu Mstaafu wakimpongeza Dean Fupe

Sunday, December 2, 2012

MKUTANO MKUU WA 31 WA KKKT-DMP ADEM BAGAMOYO

 Madhabahuni wakati wa ibada ya ufunguzi
 Mch Mzinga, Katibu Mkuu wa DMP Balozi Mariki, mke wa Askofu wa Kanisa la Kilutheri la Marekani Bi Bradosky na mke wa Mkuu wa KKKT na Askofu wa DMP Mama Erica Malasusa kwenye ibada.
 Wachungaji na wajumbe mbalimbali wa Mkutano Mkuu wa DMP, kila usharika unawakilishwa na wajumbe wawili na mchungaji.
Timu ya Sifa na kuabudu

Saturday, November 24, 2012

Upendo Fm radio katika Rural Reporting

 Kisarawe- Mji wa Kisarawe una changamoto nyingi, lakini changamoto kubwa ya kisarawe ni ukosefu wa maji. serikali inatakiwa kuangalia namna ya kutatua tatizo hili ambalo linawatesa wananchi wa Kisarawe kwa miaka nenda rudi.
 Huyu ni mmoja wa wakazi wa Kisarawe, hapa akifurahia baada ya timu ya Upendo Fm radio kumpa fedha kwa ajili ya kununulia mafuta ya taa. Kwa nyuma ni KKKT Usharika wa Kisarawe Mjini.
 Mkuu wa Jimbo la Kusini Magharibi Mch Mika Kitale akihojiwa na Isaac Kikula wa Upendo Fm kuhusu masuala mbalimbali ya Kisarawe na Jimbo lake.
 Mzee Samwel ambaye Upendo Fm ilifika nyumbani kwake kwa ajili ya kupata mawili matatu kutoka kwa mkongwe huyo wa mji wa Kisarawe. Mzee Samwel bado ana nguvu ya kuendesha baiskeli kutoka Kisarawe hadi Dar es Salaam, na tena baiskeli yake haina hata break, ni mzee mkweli na mcheshi pia.
 Jopo zima la Upendo Fm Radio likiwa nyumbani kwa mzee Samwel, Kisarawe kwa ajili ya kupata habari mbalimbali za kihistoria.
Hapa ni Meneja wa Upendo Fm Radio Bi Agatha Lema (katikati) akiwa kwenye ziara ya kutembelea wasikilizaji wa vijijini, hapa yuko Kisarawe nyumbani kwa mzee Samwel.

Thursday, November 22, 2012

HAPA NI KISARAWE HAPA-KUNA HISTORIA YA AINA YAKE

 Makaburi ya wamisionari na watumishi mbalimbali wakiwemo wachungaji wa mwanzo kabisa wa KKKT
Mji wa Kisarawe unavyoonekana kwa mbali

Thursday, November 15, 2012

JE, UMESHASIKILIZA KIPINDI CHA SAA YA BARAKA?

Sikiliza Saa ya Baraka kila siku, kuanzia saa 5 asubuhi hadi 6 kamili mchana. Kuna wengi wanabarikiwa na kipindi hiki mahiri, kinachoendeshwa na Isaac Kikula (pichani na Jacquelline Lotti Shoo. Saa ya Baraka ni gumzo la mji sasa.